Asangwile awatolea povu wanaomsema mchumba wake

Asangwile awatolea povu wanaomsema mchumba wake

Mwanamuiziki Asagwile Mwasongwe ambaye anatamba na wimbo wa ‘Ndoa’ unaofanya vizuri kupitia platform mbalimbali nchini, amewajia juu baadhi ya mashabiki ambao wamekuwa wakimsema mpenzi wake katika mitandao ya kijamii.

Utakumbuka kuwa siku chache zilizopita wakati alipokuwa kwenye mahojiano na moja ya chombo cha habari nchini, Asagwile alidai kuwa wimbo wa ‘Ndoa’ ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya mchumba wake, jambo ambalo mashabiki waliibuka na kumsema mwanammke huyo.

Akizungumza na Mwananchi Scoop leo Agosti 1, 2024 Asagwile amewatolea povu wanaomkosoa mchumba wake kwani kwa upande wake amependa kasoro wanazoziongelea.

“Kipekee niseme kwamba hakuna mwanadamu aliyekamilika na kila ambaye anatoa kosa kwa mtu na yeye atakosolewa kwa hiyo mimi sishangai komenti zao, sishangai maneno yao nimeyapokea na niseme asante kwa yote wanayoyasema.

Mimi mke wangu nampenda sana hizo kasoro zao ndio nimezichagua kwa sababu kitu pekee ambacho watu wengi hawajui ukimpenda mtu kwenye mazuri peke yake pasipo yale mabaya hii si maana ya upendo, maana ya upendo ni kuvumilia vyote kwani upendo hauhesabu mabaya, hivyo basi hayo makosa waliyoyaona kwa mke wangu ndio nimeyapenda na ndio maana tumeweza kudumu mpaka sasa miaka saba kwan hiyo ‘komenti’ zao hazinisumbui,” amesema Asagwile.

Hata hivyo, aliongeza kuwa yeye na mchumba wake huyo bado hawajafunga ndoa lakini wanaishi pamoja kama mke na mume huku wakitarajia kubariki ndoa mwezi wa kumi mwaka huu.

Katika uhusiano huo wa miaka saba, wawili hao wamebarikiwa kupata watoto wawili.

Asagwile alianza kuonekana wakati alipokuwa akishiriki shindano la kusaka vipaji vya kuimba nchini Bongo Star Search (BSS) mwaka 2023, ambapo alifanikiwa kuwa mshindi na kuondoka na kitita cha Sh 20 milioni.

Kwa sasa mwanamuziki huyo anatamba na wimbo wa ‘Ndoa’ ambao unazidi ya wasikilizaji 445,680 kupitia mtandao wa YuoTube ikiwa ni miezi miwili tu tangu kuachiwa kwake.
Kabla ya wimbo huu kumtambulisha zaidi ndani na nje ya nchi, Asagwile amekuwa akitamba na nyimbo kama ‘Kibali’, ‘Usiniache’, ‘Safari’ na ‘Leo’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags