Arnold Schwarzenegger hana mpango wa kuoa tena

Arnold Schwarzenegger hana mpango wa kuoa tena

Baada ya Muigizaji mkongwe kutoka nchini Marekani Arnold Schwarzenegger kupeana talaka na mkewe Maria Shriver mwaka 2021, inadaiwa kuwa muigizaji huyo kwa sasa hana mpango wa kuoa tena.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu cha muigizaji huyo kinaeleza kuwa Arnold hana mpango wa kufunga ndoa tena licha ya yeye na mpenzi wake Heather Milligan kuishi pamoja kama mke na mume.

Hii inakuja baada ya watu kumshuhudia mpenzi wa Arnold, Heather akiwa amevaa pete kidoleni inayosemekana kuwa huenda ikawa ya uchumba.

Arnold na Heather wamekuwa pamoja tangu 2013 katika mahusiano, ambapo wawili hao walikutana hospitali mwaka 2012 wakati Arnold alipokwenda kufanyiwa upasuaji wa bega.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags