Baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kuwa simu ikiingia katika maji ili ikauke na iwe salama inatakiwa kulala usiku mzima katika mchele lakini kampuni ya simu Apple imetoa taarifa kuwa njia hiyo siyo salama kwenye simu za Iphone huku ikiwakataza watumiaji wa simu hizo kutotumia mchele kukaushia simu zao.
Kupitia tovuti ya Apple imewakataza wateja wake kukausha simu katika mifuko ya Michele kwani kufanya hivyo kunaweza kuruhusu chembe ndogo ndogo za unga wa mchele kuharibu Iphone yako, huku ikitoa onyo kuwa njia hiyo siyo sahihi na wala haisaidii chochote.
Licha ya hayo pia imetawaka watumiaje wake wa Iphone kuepuka kutumia vifaa vyenye joto kukaushia simu zao ikiwemo Vacuums, Dryer za kukaushia nywele pamoja na kutoingiza pamba au tishu kwenye shimo za simu.
Apple imetoa namna nzuri ambayo inaweza kusaidia kuiweka salama simu yako kwa wakati huo kwa kueleza kuwa endapo simu yako itaingia maji basi piga simu yako katika kiganja cha mkono ili maji yalioyondani yaweze kutoka, kisha uiache kwenye eneo lenye hewa nzuri na usubiri kwa dakika 30 mpaka saa 24.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply