App bora ndani  ya mwezi wa Ramadhani

App bora ndani ya mwezi wa Ramadhani

Assalamu alaykum! Inafahamika kuwa kila mwaka waumini wa dini ya kiislamu hufanya ibada ya swaumu au funga ikiwa ni miongoni mwa nguzo tano za dini ya kiislamu.

Najua utakua unashangaa ukisema Ohooo! mawaidha tena? imakuaje na hapa ni smartphone tu!? Hahaha ni salamu tu hizo za mwezi mtukufu wa Ramadhani usiogope.

Leo kwenye smartphone bwana nimeamua kukuletea Application tano muhimu ambazo unaweza kuzitumia katika masiku machache yaliyobakia katika mwezi huu wa Ramadhani.

Muslim Pro –Ramadhani 2022

Naam! App ya kwanza ni hii hapa Muslim Pro ni moja kati ya app muhimu kwa muislamu yoyote yule app hii ina uwezo wa kukujulisha muda wa swala, unaweza kusoma vitabu vya Mungu na kujifunza njia za kuboresha swaumu yako kwa mwezi huu wa Ramadhani.

Muslim Dua Now –Dua & Azkar

Hii nayo ni app nyengine nzuri kuwa nayo ukiwa kama ni Muislamu kwani itakusaidia kufahamu mambo mengi yanayokuhusu ikiwemo uwezo wa kupata dua mbalimbali kwa ajili ya mambo kadha wa kadha.

 App hii inauwezo wa kukupa Dua tofauti ambazo unaweza kuzitumia pale unapokuwa na uhitaji.

Qur’an Majeed- Ramadhani 2022

Hii pia ni App nyengine itakayokujuza mengi zaidi katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, App hii inakupa uwezo wa kusikiliza Qur’an tukufu kwa haraka kabisa sambamba na hayo unaweza ukahifadhi aya Fulani kwa haraka na kwa urahisi.

Islamic Calender –Ramadhan Qur’an, Qibla, Dua

Lahaulaah! App hii pia ni nzuri katika mwezi huu na hata baada ya mwezi huu pia kwani  inakupa uwezo wa kufanya maombi kwa muda sahihi ikiwa pamoja na muda wa adhana na mambo kadha wa kadha.

Ramadhani 2022

Niko na wewe nahakikisha unapata kile unachokihitaji kupitia smartphone yako hii ni app nyengine nzuri sana ndani ya mwezi huu itakupa uwezo wa kujua muda wa dua pamoja swala katika mwezi huu  wa Ramadhani pamoja na mambo mengine mengi.

Hivyo ndivyo ninavyomaliza kwenye kipenge cha Smartphone siku ya leo kwa niaba ya magazine ya Mwananchi Scoop tunawatakia Waislamu wote Mfungo mwema wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Ramadhan Mubarackah!!!.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags