Aolewa na wanaume wawili na kuishinao nyumba moja

Aolewa na wanaume wawili na kuishinao nyumba moja

Ooooooooh! Ama kweli kuishi kwingi ndo kuona mengi, na siku zote tuliambiwa kuwa uyaone sio maghorofa ni mambo kama haya basi bwana leo katika uniqure story tunakusogezea mwanamama ambae ameolewa na wanaume wawili na kuishinao katika nyumba moja.

Kenya Stevens amefungunga kufuatia kipindi cha TLC’s new reality show na kuweka wazi kua anaishi na wanaume wawili na wanapenda sana

Mwanamama huyo alieleza Kwamba yeye na mume wake wa kwanza Carl Stevens waliamua kufanya hivyo baada ya  Kenya kumueleza mume wake kuwa amekutana na mwanaume mwingine na anampenda sana.

Aliendelea kueleza kwa kusema kuwa swala hilo lilikuwa gumu sana kwa mumewe kulikubali kwa haraka na ilichukua miaka miwili mpaka hapo mume wake kukubaliana na wazo hilo la  mke wake kuongeze mume wa pili.

Carl na Kenya katika ndoa yao yenye Zaidi ya miaka 30 walibahatika kupata watoto watatu na kuwaeleza juu ya uwamuzi walio huo na watoto hawakuwa na pingamizi walikubali.

Kenya alifunga ndoa nyingine na mume wake mpya Tiger na wanaishi kwenye nyumba moja,  na wote kwa pamoja wameeleza kuwa wanaamani sana, na imeelezwa kuwa licha ya kuishi pamoja katika nyumba moja lakini Carl ameoa mwanamke mwingine na mume wa pili pia anamahusiano mengine nje ya muunganiko wa ndoa waliokuwa nayo.

Mmmmmmh! swali la kujiuliza wadau wangu je mwanamama huyu amewezaje maana, wapo ambao wameoa wanawake wawili, watatu na wameshindwa kuwafanya waishi katika nyumba moja, embu dondosha komenti yako utueleze mtazamo wako katika hili.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags