Aoa wake 7 kwa mpigo, Huku bibi harusi wawili wakiwa ni ndugu

Aoa wake 7 kwa mpigo, Huku bibi harusi wawili wakiwa ni ndugu

Mwanaume mmoja ambaye ni mfanyabiashara maarufu kutoka nchini Uganda anayefahamika kwa jina la Ssaalongo Nsikonenne Habib amezua gumzo kupitia mitandao ya kijamii baada ya kufunga ndoa na wanawake saba siku moja.

Habib aliwaoa wanawake hao saba, huku wawili wakiwa ni ndugu wa tumbo moja ambapo wanawake hao walitambulika kwa majina Mariam, Madina, Aisha, Zainabu, Fatuma, Rashida, na Musanyusa ambaye ni mke wa kwanza wa Habib na amedumu naye kwa miaka saba, harusi iliyofanyika katika kijiji cha Bugereka wilayani Mukono Jumapili, Septemba 10, 2023.

Licha ya mfanyabiashara huyo kufanya tukio hilo la ndoa ambalo limewashangaza wengi huku wakisema kuwa ni mara ya kwanza kwa tukio hilo kutokea, mfanyabiashara huyo aliwanunulia magari mapya wake zake wote kama zawadi.



Bwana harusi huyo alitoa maelezo kwa kuwapongeza wake zake kwa kuwa waaminifu kwake. Amesema, "Wake zangu hawaoneani. Niliwatambulisha kando na kuamua kuwaoana wote mara moja ili kutengeneza familia kubwa yenye furaha," alisema.

Kwa mujibu wa baba yake bwana harusi, Hajj Abdul Ssemakula, amedai ndoa ya wake wengi imekuwa ni desturi katika familia hiyo akiongezea kuwa babu yake alikuwa na wake sita aliyoishi nao katika nyumba moja. Inasemekana  Habib alivunja rekodi ya kuoa wake wengi nchini Uganda kwa wakiti mmoja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags