Antony atolewa ‘timu’ ya taifa kwa madai ya kumpiga ex wake

Antony atolewa ‘timu’ ya taifa kwa madai ya kumpiga ex wake

‘Winga’ kutoka ‘klabu’ ya Manchester United Antony ameondolewa kwenye kikosi cha ‘timu’ yake ya Taifa ya Brazil kwa kosa la kumshambulia mpenzi wake wa zamani Gabriela Cavallin.

Shirikisho la ‘soka’ Brazil limefanya maamuzi hayo baada ya mwanadada huyo kudai kuwa alishambuliwa na mchezaji huyo kwa nyakati tofauti kati ya Juni 2022 na Mei 2023.

Gabriela anadai kuwa aliumizwa kifuani na kulazimika kufanyiwa upasuaji ambapo askari wa Sao Paulo na Greater Manchester wanaendelea na uchunguzi wa matukio hayo.

Aidha mchezaji huyo amekanusha kwa kusema kuwa uhusiano wao ulikuwa na misukosuko mingi lakini hakuwahi kumpiga na hizo ni taarifa za kutungwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags