Antonio Brown aachiwa kwa dhamana

Antonio Brown aachiwa kwa dhamana

Baada ya mchezaji wa zamani wa NFL, Antonio Brown, kukamatwa na kuwekwa jela toka Jumapili ya wiki iliyopita kwa kosa la kutolipa pesa ya matumizi kwa watoto wake, hatimaye ameachiwa huru kwa dhamana.

Inaeleza kuwa Wiltrice Jackson  ambaye ni mzazi mwenzie mchezaji huyo alifungua mashitaka na kutaka akamatwe kutokana na kutojitambua huku akieleza kuwa Brown anadaiwa zaidi ya $30,000 za malezi ya mtoto.

Hata hivyo kutokana na kuachiwa kwake Polisi katika jimbo hilo wameeleza kuwa Brown aliachiliwa baada ya kutoa dhamana ya $15,000 ambayo ni zaidi ya tsh 37 milioni. Wawili hao wana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 aitwaye Antanyiah.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BirudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags