Angelina Jolie amshtaki aliyekuwa mumewe Brad Pitt

Angelina Jolie amshtaki aliyekuwa mumewe Brad Pitt

Mwigizaji maarufu nchini Marekani Angelina Jolie amefungua shauri mahakamani akimshutumu mumewe wa zamani, mwigizaji mwenzake Brad Pitt kwa kumshambulia yeye na watoto wao kwa ulevi wakati wa safari ya ndege ya kibinafsi na kumfanya aombe talaka,

Jolie anasema Pitt alimsukuma  na kuwashambulia watoto wao wawili huku akitukana na kuwamwagia pombe wakati wa safari ya kutoka Ufaransa kuelekea Los Angeles mwaka 2016, madai yaliyopingwa vikali na Bwana Pitt.


Wawili hao walidumu kwenye mahusiano kwa muda wa miaka 10 kabla ya kuchumbiana mwaka 2012 na kuoana mwaka 2014 na hatimaye kutalikiana Septemba 2016.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags