Anayedaiwa kumpiga MohBad atafutwa, Donge nono kutolewa  atakaye mpata

Anayedaiwa kumpiga MohBad atafutwa, Donge nono kutolewa atakaye mpata

Jeshi la ‘polisi’ nchini Nigeria bado linaendelea kukusanya uchunguzi kufuatia kifo cha msanii MohBad ambapo jeshi hilo limetoa tangazo la kukamatwa kwa kijana Owodunni Ibrahim A.K.A. Prime Boy ikiwa ni baada ya kushindwa kutokea ‘polisi’ kusaidia uchunguzi.

Prime Boy kufutia wito huo hakutokea na wala hajulikani alipo kwasasa, hivyo basi jeshi hilo la polisi limetoa ‘ofa’ ya zaidi ya 3 milioni kwa atakayetoa taarifa kamili itakayo pelekea kukamatwa kwa mtu huyo.

Jeshi linamsaka kijana huyo anayedaiwa kumjeruhi MohBad kwenye party huko Ikorodu siku hiyo aliyofariki msanii huyo, licha ya Prime Boy kukanusha kumpiga MohBad.

Taarifa hiyo ya polisi imeeleza “Prime Boy ni mrefu mweusi ana alama za kitamaduni za kabila la Yoruba, eneo lake la mwisho kuonekana ni linalojulikana ni 3rd power, Okeeletu huko Ikorodu, Nigeria”
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags