Amuua Mkewe kisa Elfu 10

Amuua Mkewe kisa Elfu 10

Duuuuuh! Kila siku matukio ya ajabu yanazidi kuongezeka moja ya tukio la kuskitisha Zaidi ni Jeshi la polisi mkoani Manyara linamshikilia Petro Basso (38) mkazi wa Gabadaw wilayani Babati mkoani Manyara kwa kosa la kumpiga mkewe Maria Sakware (49) kwa fimbo na kumsababisha kifo huku chanzo kikielezwa kuwa mtuhumiwa kumtuhumu mkewe amechukua pesa yake kiasi cha shilingi elfu 10.


Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Manyara ACP Benjamin Kuzaga wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi la polisi mkoani Manyara.

Kuzaga amesema kuwa kiini cha tukio hilo ni Ulevi wa mume wa marehemu na kumtuhumu marehemu kuwa amechukua pesa yake shilingi elfu 10 na kuanza kuchukua hatua mkononi kwa kumchapa na fimbo na kumsababishia majeraha mwili mwake ikiwemo maumivu katika mguu wake wa Kushoto pamoja na kumvunja mkono wa kushoto.

Marehemu alifikishwa katika kituo cha Afya cha Bashnet kwa ajali ya kupata matibabu na ndipo umauti ulipomkuta.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kusababisha kifo cha mkewe na upelelezi utakapokamilika atafikishwa katika vyombo vya sheria.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags