Amuua Mama yake kisha Amkata Koromeo

Amuua Mama yake kisha Amkata Koromeo

Daaaah huu ni mtihani mkubwa sana unaoisumbua dunia kwa sasa kijana mmoja kutoka nchini Uingereza amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada kukubali kuhusika na mauaji ya mama yake mzazi.

Kijana mwenye umri wa miaka 19 anayetambulika kwa jina la  Aaron Matthew alimuua mzazi wake wa kike  kwa kumchoma visu zaidi ya mara 80 kisha kumkata sehemu ya koo.

Aidha Kijana huyo alimuua Mama yake aliyefahamika kwa jina la  Ingrid Matthew mwenye umri wa miaka 54 kabla ya kumkata koo kisha kumtelekeza chumbani na kumuacha afariki.

Hata hivyo mara baada ya kutekeleza tukio hilo Aaron Matthew alijipeleka mwenyewe katika kituo cha Polisi cha Cambridgeshire siku moja baada ya mwili wa marehemu kugundulika.

Sambamba na hayo inasemekana kuwa mtu aliyefanikiwa kugundua mwili wa mwanamke huyo ni mumewe wa zamani ambaye alikuwa ameshatengana naye ambaye pia ni Baba mzazi wa Aaron Matthew aitwaye Andrew Marshall.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags