Aliyezikwa hai alamba dili Amazon Prime video

Aliyezikwa hai alamba dili Amazon Prime video

Mtengeneza maudhui kutoka nchini Marekani Mr Beast ambaye alijulikana zaidi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuzikwa akiwa hai kwa siku saba, hatimaye amelamba dili nono kutoka Amazon Prime Video.

Mr Beast ameripotiwa kusaini mkataba wenye thamani ya dola 100 milioni na Amazon Prime kwa ajili ya kurusha kipindi chake cha kwanza mwaka huu kwenye runinga.

Onesho hilo, ambalo bado halijathibitishwa rasmi na Amazon, inadaiwa kuwa episode ya kwanza inatarajiwa kurushwa katika chaneli ya YouTube ya Mr Beast kabla ya kuoneshwa kwenye jukwaa la Prime Video, kwa lengo la kuhamisha watazamaji wake kutazama kwenye runinga.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags