Aliyezaa na Barakah The Prince afunguka

Aliyezaa na Barakah The Prince afunguka

Aisee hii nayo kubwa kuliko Msanii wa filamu aliyezaa mtoto na Barakah The Prince, Careen Simba anasema kuwa  chanzo cha kuachana na msanii huyo ni kuanzisha mahusiano na Naj wakati akiwa na ujauzito wake.

Careen Simba ambaye pia ni video vixen ametoa yamoyoni wakati akihojiwa na kituo kimoja cha Televisheni na kuzungumza mambo kadha wa kadha.

"Mimi na Barakah tulijuana muda mrefu sana, mimi mpaka nabeba mimba tukaachana na Barakah na kuzinguana kwa sababu ya Naj, sikuwa mchepuko nilikua mwanamke wake". 

Careen ameongeza kusema wakati yupo kwenye mahusiano na Barakah hawakutaka kuweka wazi kwa sababu hapendi mambo ya kujulikana sana. 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags