Aliyewahi kuwa mpiga Besi wa bendi ya Bob Marley afariki

Aliyewahi kuwa mpiga Besi wa bendi ya Bob Marley afariki

Aliyekuwa mwanamuziki wa nyimbo za #Raggae kutoka nchini Jamaica #AstonBarrett, maarufu kama ‘Family Man’ amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77.

Mwanamuziki huyo aliwahi kupata umaarufu nchini humo na duniani kote akiwa kwenye Bendi ya #Upsetters, iliyokuwa chini ya mwanzilishi mmoja wa Reggae Lee ‘Scratch’.

Pia mwaka 1994 alijiunga na bendi ya marehemu Bob Marley (Bob Marley and the Wailers) akiwa kama mpiga besi (bassist) wa bendi hiyo, alikuwa mmoja wa watu waliochangia sana kukua kwa Reggae.

Barrett yupo kwenye kila albumu ya Bob ‘Wailers’, pamoja na kufanya kazi na wanamuziki maarufu kama Burning Spears, Peter Tosh .

Baadhi ya nyimbo maarufu ambazo aliwahi kuwemo akiwa kwenye bendi ya Bob Marley  ni pamoja na  ”Get up Stand Up, Stir It Up, No Woman, No Cry na  Could You Be Love”.

Family Man alizaliwa mwaka 1946  Kingston nchini Jamaica  na kufariki mwaka 2024, kutokana na matatizo ya kiafya aliyokuwa akipambana nayo kwa muda mrefu ambayo familia yake haikutaka kuyaweka wazi.

Taarifa za kifo chake zilitolewa na mtoto wake wa kiume aitwaye Barrett Jr siku ya Jumamosi kupitia mitandao ya kijamii, ambapo aliandika, “ Kwa moyo mgumu tunatoa taarifa ya kufariki kwa mpendwa wetu Aston 'Familyman' Barrett baada ya kupambana na matibabu kwa  muda mrefu."
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags