Aliyepandikizwa chipu kwenye ubongo aanza kutumia kompyuta

Aliyepandikizwa chipu kwenye ubongo aanza kutumia kompyuta

Ukuaji wa teknolojia unazidi kushangaza wengi ambapo kwa sasa binadamu amefanikiwa kupandikizwa chipu kwenye ubongo kwa ajili ya kutumia kompyuta kwa kuwaza tu.

Ni siku chache zimepita tangu bilionea Elon Musk kutangaza kufanikiwa kupandikiza chipu kwenye ubongo wa mwanadamu kwa ajili ya kutumia kama kompyuta hatimaye amedai chipu hiyo imeanza kufanya kazi.

Musk kupitia kampuni ya Neuralink amesema mtu huyo kwasasa anaweza kutumia kipanya ‘mouse’ cha kompyuta kwa kutumia mawazo ya ubongo.

“Maendeleo ni mazuri, mtu huyo amepata ahueni kamili na ana uwezo wa kudhibiti kipanya, kusogeza kipanya kwenye skrini kwa kufikiria tu, na kwasasa anaendelea vizuri hakuna mdhara yoyote aliyoyapata” Musk, amebainisha kwenye mtandao wa X.

Teknolojia ya Neuralink inafanya kazi kupitia chipu hiyo ya kisasa yenye ukubwa wa sarafu tano zilizopangwa ambazo huwekwa ndani ya ubongo wa binadamu kupitia upasuaji.

Lengo lake ni kuwasiliana na kompyuta moja kwa moja na ubongo teknolojia ambayo itawasaidia watu wenye matatizo ya kupooza.

Mwaka jana kampuni inayotekeleza hilo ilipokea idhini kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA), kwa ajili ya kufanya jaribio lake la kwanza ambapo ilitangaza kutafuta watu wa kujitolea kupandikizwa.

Je teknolojia hii ikifika nchini uko tayari kupandikizwa?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post