Aliyembaka mwanaye na kumzalisha ahamishwa gereza

Aliyembaka mwanaye na kumzalisha ahamishwa gereza

Mahakama nchini Austria imeidhinisha mfunguwa Josef Fritzl (89) aliyembaka binti yake na kumzalisha watoto saba kuhamishwa gereza baada ya tabia yake kubadilika.

Inaelezwa kuwa mzee huyo alikuwa akimfanyia binti yake ambaye jina lake lilihifadhiwa udhalilishaji wa kijinsia kwa kumbaka mara kwa mara ambapo alimfungia ndani ya nyumba kwa zaidi ya miaka 24 na kumzalisha watoto saba.

Mwaka 2019 Fritzl alifungwa kifungo cha maisha na kuswekwa kwenye jela ya watu hatari, iitwayo Krems katika mji wa Vienna nchini humo ambapo kwa sasa atapelekwa kwenye gereza la kawaida kwa sababu sio mtu hatari tena ingawa atakuwa katika kitengo cha magonjwa ya akili.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags