Aliyekuwa kocha wa Mamelod atimkia Wydad

Aliyekuwa kocha wa Mamelod atimkia Wydad

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Mamelod Sundowns, Rulani Mokwena ameripotiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kama kocha mkuu katika timu ya Wydad Casablanca.

Inaelezwa kuwa Mokwena anatarajia kuwasili leo katika nchi ya Morocco kwa ajili ya kuanza kuitumikia timu hiyo. 

Hii ni baada ya kuondoka kwake ghafla katika klabu ya Mamelod kutokana na kuingiliwa majukumu yake na kutofurahishwa na kitendo cha timu hiyo kumpa thamani Mkurugenzi wa Michezo Flemming Berg, katika usajili wa wachezaji.

Utakumbuka kuwa ‘kocha’ huyo mwenye umri wa miaka 37 aliiambia Mamelod kama hawatompa uhuru wa kuitengeneza ‘timu’ basi atajiweka kando na ‘timu’ hiyo.

Kocha huyo mchanga, ambaye aliiongoza Sundowns kutwaa mataji mfululizo ya DStv Premiership na taji la kwanza la Ligi ya Soka ya Afrika (AFL).
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post