Aliyekuwa akipumulia mashine kwa miaka 72 afariki dunia

Aliyekuwa akipumulia mashine kwa miaka 72 afariki dunia

Aliyekuwa mwanasheria ambaye amekuwa akipumulia mashine ya mapafu kwa zaidi ya miaka 70 aitwaye Paul Alexander amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78, Machi 11 mwaka huu.

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na kaka yake Philip kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo ali-share picha akiwa na ndugu yake huyo huku akieleza jinsi alivyoishi na Paul kuhusiana na ucheshi wake vitu alivyokuwa akipenda vikiwemo kula chakula kizuri, mvinyo, wanawake, kuzungumza kwa muda mrefu pamoja na kucheka.

Ikumbukwe kuwa Paul aliugua Polio akiwa na umri wa miaka 6 mwaka 1952 ambao ugonjwa huo ulimpelekea kupooza na mapafu yake kuharibika hivyo alilazimaki kutumia kifaa cha chuma kwa ajili ya upumuaji (Iron Lung).

Hata hivyo Paul kutokana na kuishi kwa muda mrefu akipumulia mapafu ya chuma ilipelekea kuingia katika kitabu cha rekodi cha dunia Guiness World Record, kwa kuwa mtu wa kwanza aliyepumulia mapafu ya chuma kwa muda mrefu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post