Aliyekosa nafasi ya urais 2022 achomwa kisu

Aliyekosa nafasi ya urais 2022 achomwa kisu

Kiongozi wa Upinzani nchini Korea Kusini amechomwa kisu katika mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika katika mji wa Busan nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari la Kimataifa la Yonhap la nchini humo imeeleza Lee Jae-myung ambaye alikosa nafasi ya Urais wakati wa uchaguzi Mkuu wa Urais mwaka 2022 amechomwa kisu upande wa kushoto wa shingo yake mapema asubuhi ya leo, Jumanne Januari 02,2024

Hata hivyo aliyefanya shambulizi hilo amekamtwa na anakadiriwa kuwa na miaka kati ya 50 na 60, ambapo inaelezwa kuwa alikuwa amemkaribia Lee ili kumuomba saini yake, kabla ya kumchoma kwa kisu hicho, hadi sasa bado hakuna taarifa kuhusiana na maendeleo ya afya yake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags