Aliyehusika mauaji ya Pop Smoke aachiwa huru

Aliyehusika mauaji ya Pop Smoke aachiwa huru

Kati ya watuhumiwa wanne walioshitakiwa katika mauaji ya ‘rapa’ wa Marekani J. Christopher Smith maarufu #PopSmoke ameripotiwa kuachiwa huru kutoka jela, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 4 na miezi 2.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ imeeleza kuwa Smith alhukumiwa kifungo hicho baada ya kukiri kuhusika na kifo cha ‘rapa’ huyo lakini kifungo chake kimekuwa cha muda mfupi kwa sababu anadaiwa kuwa alifanya mauaji hayo akiwa na umri wa miaka 15.

Hata hivyo Christopher Smith amethibitisha hilo kwa kuweka picha katika Insta Stori yake kuonesha kuwa yupo huru kwa sasa.

Ikumbukwe kuwa rapa Smoke aliauwa kwa kupigwa risasi jijini Los Angles Februari 19, 2020.

Rapa huyo aliwahi kutamba na ngoma kama Dior, Mood Swings, Got it on Me, Welcome to the Party, Hello, The Woo na nyingine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags