Aliyeahidiwa cherehani na Rais Samia afunguka

Aliyeahidiwa cherehani na Rais Samia afunguka

Unaweza kusema ni asubuhi ya kheri kwa Beatrice Mwalingo (28) fundi nguo ambaye amepewa ahadi ya kununuliwa cherehani na Rais Samia Suluhu Hassan.

Hiyo ni baada ya dada huyo ambaye anafanya kazi ya ushonaji kwa miaka mitano sasa kuomba zawadi ya Cherehani kutoka kwa Rais Samia kupitia ukurasa wa kiongozi huyo.

Katika chapisho la Rais Samia kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika juu ya kuwasili kwake nchini Indonesia kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3, kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo.



“Uhusiano wa Tanzania na Indonesia ambao mapema mwezi huu (Januari 13) ulitimiza miaka 59, umekuwa wenye tija kwa nchi yetu na mamilioni ya Watanzania hasa kwenye kilimo na biashara. Tunaendelea kuifanya kazi ya kukuza uhusiano huu ili kuleta tija zaidi kiuchumi kwa nchi yetu,” aliandika Rais.

Hatahivyo, Beatrice yeye pasipokujua itakuwa siku yake ya bahati aliacha ujumbe chini ya chapisho hilo uliosomeka. “Sawa mama. Ukiwa unarudi nyumbani naomba uniletee zawadi ya Cherehani,” aliandika.

Muda mchache baadaye Rais Samia alijibu ujumbe wake na kumuambia. “Hujambo, Beatrice? Nimepata wasaa wa kuusoma ujumbe wako. Hongera kwa kazi na kujituma. Wasaidizi wangu watawasiliana na wewe kukusaidia upate mashine uliyoomba kwa shughuli zako. Nakutakia kila la kheri.

Akizungumzia na Mwananchi suala hilo, Beatrice amesema hakudhani kama ingeweza kutokea au kuahidiwa kitu na kiongozi wa nchini huku akieleza kuwa pindia atakapopata cherehani hiyo itakuwa ni mwanzo wa kuwezesha vijana wengine ili wajikwamue kimaisha.


"Ukweli siku ya jana wakati nimekaa nilisema ngoja niombe cherehani kwa mama, na kweli sikutegemea kama nitajibiwa, ukweli nimefurahi sana ni kitu ambacho kimenipa furaha na 'motivesheni' kwenye kazi zangu zaidi.


Beatrice anasema taarifa za kujibiwa na Rais Samia alizipata mida ya saa 12 kasoro kutoka kwa rafiki yake lakini hakutaka kumuamini hadi alipoona mwenyewe.

Licha ya kujibiwa anasema kuwa bado hajatafutwa lakini anaamini watafanya hivyo kwani muda bado. Anamaliza kwa kuwashauri watu kujaribu kueleza changamoto zao kwenye post za viongozi kwani hawawezi kujua bahati zao.


Hadi sasa Beatrice anamika minne tangu aanze kufanya kazi za ushonaji, mwanzo alikuwa akifanya nchini Japan, lakini tangu mwaka jana mwezi wa Novemba anafanyia nchini Tanzania.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags