Alikiba ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza ambae sio Mnigeria kushinda Tuzo ya NXT Honours Life Time Archievement Award (Tuzo ya mafanikio ya maisha Afrika) ambapo kwa miaka yote hii tuzo imekua ikibebwa na wasanii kutokea Nigeria.
Mkurugenzi mkuu wa tuzo hizo anaefahamika kama Moma wakati akimtangaza Kiba kama mshindi wa tuzo hiyo amesema michango ya Alikiba kwenye muziki wa Afrika inazidi nyimbo ambazo ametoa huku akiendelea kusimama kwenye aina moja ya muziki.
“Michango ya Alikiba kwenye muziki wa Afrika inazidi nyimbo alizotoa amekuwa na nguvu ya kitamaduni kuziba pengo kati ya bara zima la Afrika huku akibakia mkweli kwenye Muziki wa Bongofleva inafaa kutambua urithi wa heshima yetu kama Afrika,” amesema Moma.
Tuzo ya mwisho ya NXT Honours Life Time Archievement Award alishinda DON JAZZ ambae ni msanii na producer lakini pia mkongwe na anamchango wake mkubwa katika ukuaji wa Afrobeats hususani kuwashika mkono wasanii kwa kuwatoa chini mpaka kutambulika Duniani kwa kuanzisha Lebo ya Mavin Record ambayo imebeba nyota wakubwa kwenye muziki wa Afrika wasanii kama Rema, Ayra Starr na wengineo.
Leave a Reply