Alicho sema Shetta baada ya mtoto wake kushinda

Alicho sema Shetta baada ya mtoto wake kushinda

Mwanamuziki wa #BongoFleva, #Shetta ameweka wazi kuwa mtoto wake #Qayllah ambaye jana amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi CCM Taifa hakupata uongozi huo ghafla, alianza kuipenda CCM tangu akiwa na miaka mitatu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyo ali-post video ikimuonesha #Qayllah akiwa na umri wa miaka mitatu akiimba wimbo wa CCM, huku akiandika ujumbe usemao mtoto wake hajawa kiongozi ghafla, bali chama kilimuandaa tangu akiwa mdogo.

#Qayllah amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi #CCM Taifa baada ya kupata ushindi katika Mkutano Mkuu wa Chipukizi Taifa uliofanyika Disemba 20, 2023 kwa kupata kura 303.








Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags