Albamu ya Zuchu mbioni kutoka

Albamu ya Zuchu mbioni kutoka

Baada ya mzalishaji muziki nchini Trone, kuthibitisha ujio wa albamu ya mwanamuziki wa Bongo Fleva Zuchu, sasa msanii huyo amesema imekamilika kwa asilimia 100.

Zuchu ametoa taarifa inayoeleza kuwa albamu yake imekamilika kwa asilimia mia moja, ingawa bado hajataja tarehe rasmi ya kuachiwa

Utakumbuka Mei 28 mwaka huu Trone alishare video akiwa na Zuchu studio iliyoambatana na ujumbe ukieleza kuwa yeye na Zuchu wametengeneza albumu itakayosumbua spika za watu ambayo itatoka hivi karibuni.

Endapo albumu hiyo itafanikiwa kuachiwa itakuwa ya kwanza kwa Zuchu. Mwaka 2020 mwanamuziki huyo alifanikiwa kutoa EP yenye nyimbo saba ambayo ndiyo iliyomleta mjini.

EP hiyo ya Zuchu iliyopewa jina la ‘I Am Zuchu’ ilikuwa na nyimbo kama ‘Hakuna Kulala’, ‘Nisamehe’, ‘Wana’, ‘Ashua’, ‘Kwaru’, Raha’ na ‘Mauzauza aliyomshirikisha Mama yake Khadija Kopa.

Zuchu kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Siji’ alichomshirikisha Toss ambacho kinafanya vizuri kupitia mitandao ya kijamii huku ikishika namba sita kupitia mtandao wa YouTube.

Ikumbukwe kuwa Zuchu alitambulika rasmi kwenye Tasnia ya muziki Aprili 2020 baada ya kusainiwa chini ya lebo ya WCB Wasafi Records inayomilikiwa na mwanamuziki Diamond Platnumz.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags