Al Pacino akataa ujauzito wa mpenzi wake

Al Pacino akataa ujauzito wa mpenzi wake

Wiki hii bana kumekuwa na mambo mengi sana baada ya mpenzi wa kikonge muigizaji Al Pacino kuonekana kuwa na ujauzito na mzee huyo kutarajia kupata mtoto wa nne, hivi karbuni kupitia mitandao mbalimbali nchini Marekani imeripoti kuwa muigizaji huyo wa filamu haitaji mtoto.

Tetesi zinaeleza kuwa mzee huyo sababu kubwa ya kuachana na wapenzi wake wa awali hakutaka kuongeza mtoto mwingine, na kueleza kuwa mimba hii ya mpenzi wake wa sasa Noor Alfallah haikuwa kwenye makubaliano yao.

Imedaiwa kuwa mawakili wa Al Pacino wanataka mtoto akizaliwa apimwe DNA, huku binti huyo akiwa na maswali ya kujibu kuhusu kuficha ujauzito kwa miezi mitatu bila kumwambia mtu, ata ndugu zake.

 Al Pacino alishangazwa sana na taarifa za ujauzito kutoka kwa mpenzi wake baada ya kuwa nae kwenye mahusiano kwa mwaka mmoja tu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags