Al B aomba uchunguzi ufanyike, kifo cha ex wa Diddy

Al B aomba uchunguzi ufanyike, kifo cha ex wa Diddy

Mwanamuziki wa Marekani Al B. Sure ambaye pia ni mzazi mweza wa Kimberly Porter ameiomba mahakama kufanya uchunguzi upya kuhusiana na kifo cha mwanadada huyo ambaye pia alikuwa mpenzi wa zamani wa Diddy.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Sure ametoa wito wa uchunguzi juu ya kifo cha ghafla cha Kim huku akidai kuwa uchunguzi huo uelekezwe kwa waliokuwa wakifanya kazi na Kim pamoja na waandishi wa habari.

“Ninaandika chapisho hili rasmi kuomba uchunguzi kuhusu kundi zima la watu waliofanya kazi au walikuwa karibu na makazi ya Bi. Kimberly Porter, ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari waliotoa msaada wa kuandika barua hii.

"Imenijia habari kwamba watu hawa waliagizwa kuiba kompyuta na vifaa vya simu vya Porter, ambavyo vilikuwa na “maandishi ya awali ya kitabu chake.” Maandishi ya awali yanatofautiana na upuuzi uliotengenezwa na kurasa za kukera zilizosambazwa kupitia Amazon zinazoonyesha vitendo vya kingono vya wazi vinavyonihusisha, ambavyo havijawahi kutokea na vilihaririwa na kuongezwa baada ya mauaji ya kusikitisha ya Bi. Porter.” Amemandika Al B. Sure

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinadai kuwa Sure ameibua sakata hilo upya kufuatia na kukamatwa kwa Diddy ambaye anashikiliwa kwa makosa matatu likiwemo la biashara ya ngono.

Utakumbukwa kuwa mwaka 2022, Sure ambaye alitamba na ngoma ya ‘Nite and Day’ aliwahi kudai Diddy alihusika kwa asilimia mia kwenye ugonjwa wake, hivyo anaamini Kim aliuawa kwa sababu alikuwa na mipango ya kufichua uhalifu aliokuwa akiufanya Combs ukiwemo bishara ya binadamu.

Combs na Kim Porter walikuwa kwenye mahusiano kwa takribani miaka 10 huku wawili hao wakifanikiwa kupata watoto wawili mapacha ambao ni D'Lila Combs na Jessie Combs waliozaliwa mwaka 2006.

Kim Porter alifariki tarehe 15 Novemba, 2018, huko Toluca Lake, California kutokana na Nimonia ya Lobar baada ya siku kadhaa za kuwa na dalili ya mafua.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags