Akon: Kama unamawazo ya kumiliki ndege binafsi yafute haraka

Akon: Kama unamawazo ya kumiliki ndege binafsi yafute haraka

Mwanamuziki mkongwe na Mfanyabiashara kutoka nchini Marekani  #Akon amefunguka kuhusu uzoefu wake wa kumiliki ndege binafsi, kwa maoni yake anadai kuwata wenye mawazo na shauku ya kumiliki ndege waache mara moja.

Nakusema kuwa yeye aliwahi kujaribu kumiliki ndege binafsi lakini haikuchukua muda ndege hiyo ilidumu kwa miezi 6 na aliiuza haraka sana.

Akon alieleza hayo katika mazungumzo na Logan Paul (Impaulsive) ambapo alisema kwamba chochote unachofanya ila usiwahi kumiliki ndege binafsi kwani gharama za kuihudumia ndege hiyo kwenye matengenezo inakuwa zaidi ya bei ya kununulia ndege mpya.

Akon ameeleza hayo kwani imekuwa ndoto ya watu wengi kumiliki ndege binafsi bila ya kufahamu kuwa kuna gharama kubwa ya kuihudumia ndege hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags