Akon fichua siri namna ya kuwa bilionea

Akon fichua siri namna ya kuwa bilionea

Mwanamuziki Akon ameeleza namna ambavyo wamarekani wenye asili ya kiafrika wanaweza kuwa mamilionea ikiwa tu watawekeza kikamilifu barani Afrika.

Akon ameyasema hayo kwenye mahojiano yake na podcast ya Revolt “Assets Over Liabilities," kuwa mtazamo wake ni kwamba Afrika ina kila kitu na mara nyingi vitu kutoka Afrika vinategemewa nchini Marekani, hivyo basi wamarekani wenye asili ya kiafrika wasijifikirie mara mbili wawekeze Afrika ili wafanikiwe.

Mkali huyo aliendelea kwa kueleza kuwa watu weusi ndiyo wanaoendesha ulimwengu, bila Afrika Marekani inayumba kwa hivyo wanapaswa kuizingatia na sio pesa zote kuwekeza Marekani kwani kwenye upande wa Afrika kuna kila kitu.

Na huwezi gusa sekta yoyote bila kulitaja bara hilo, akatolea mfano wa sekta kama kama fashion, madawa, michezo, burudani, nidhamu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags