Akon akanusha madai ya kumbaka binti wa miaka 13

Akon akanusha madai ya kumbaka binti wa miaka 13

Baada ya mtayarishaji mkongwe wa muziki kutoka nchini #Marekani, #SugeKnight kudai kuwa mwanamuziki na mfanyabiashara #Akon, aliwahi kumbaka binti wa miaka 13, hatimaye mwanamuziki huyo amekanusha madai hayo.

Kufuatia mahojiano yake na #TMZ, #Akon amekanusha madai hayo na kusema kuwa madai hayo ni ya uongo na yanamchukiza sana huku akiweka wazi kuwa yuko mbioni kufanya kikao na ‘timu’ yake ya wanasheria kwa ajili ya kumfungulia ‘kesi’ #Suge ya kumkashifu mwanamuziki huyo.

#SugeKnight, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 28 jela kwa kuua bila kukusudia, aliyasema hayo kupitia #Podcast mpya ya ‘Collect Calls’ ambayo imezinduliwa na #Knight kutoka gerezani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags