Ajuta kufanya upasuaji, Anaishi kama mtoto

Ajuta kufanya upasuaji, Anaishi kama mtoto

Mwanamke mmoja kutoka Uingereza anayefahamika kwa jina Lea Lazaro ajutia kufanya upasuaji wa mwili wake wote ambao umepelekea kurudi kama mtoto na baadhi ya maumbile yake kuharibika siku hadi siku.

Mwanamke huyo mwenye watoto wawili anaeleza kuwa maisha yake tangu afanye upasuaji yamekuwa ya shida na anatumia gharama kubwa kuweka mwili wake sawa hasa tumbo lake ambalo limeharibika na kubaki ngozi nyepesi ya mwili wake. Lea anajiona kama amebakiwa na mifupa iliyo funikwa na ngozi iliyo kauka yenye michirizi. 

Kwa sasa ana umri wa miaka 39 lakini huvaa nguo za mtoto wa miaka 12 na anajiona kama kituko, lakini hakuweza kusema aina gani ya upasuaji na wapi alipo fanya upasuaji huo.

Changamoto nyingine anayopata ni kula kiasi kidogo cha chakula kama mtoto kutokana upasuaji wa tumbo anajihisi kuwa na hatia kwa kufanya upasuaji huo.
.
.
.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags