Ajiteka ili apate pesa kwa mjomba wake

Ajiteka ili apate pesa kwa mjomba wake

Kijana Nafiu Sulaiman mwenye umri wa miaka 19, amekamatwa na polisi baada ya kujiteka nyara yeye mwenyewe na kukusanya fidia ya Zaidi ya million moja ya kitanzania kutoka kwa mjomba wake katika jimbo la Kano nchini Nigeria.

Kulingana na chombo cha habari cha Daily Trust kimeeleza kuwa, Sulaiman alikuwa akifanya kazi chini ya mjomba wake katika duka la saruji (cement) katika kijiji cha Garindau katika eneo la serikali ya mtaa la Warawa.

Kamishna wa Polisi wa jimbo hilo, Muhammad Usaini Gumel, ambaye alithibitisha kukamatwa kwa Sulaiman, alisema kijana huyo alikamatwa wakati wa uchunguzi.

Gumel alieleza kuwa mtuhumiwa alikiri kwamba alijiteka nyara mwenyewe ili kupata pesa kutoka kwa mjomba wake.

Akizungumza baada ya kukamatwa, kijana huyo alikiri kwamba alipanga kujiteka nyara mwenyewe na alikaa katika jengo lililokuwa bado halijakamilika kwa siku kadhaa.

Aliongeza kuwa alijiteka nyara ili apate pesa za kununua nguo na vitu vingine, lakini pesa za fidia ziliibiwa kutoka kwake.

"Nilipanga kila kitu nilitumia simu kwa kutumia namba nyingine kumwita bosi wangu, ambaye pia ni mjomba wangu, nilidai fidia na kuwaomba wailete mahali Fulani, nilikaa huko kwa muda mrefu, na nilipohitaji chakula, nilitoka kununua na kurudi. Lakini sikuutumia hata asilimia moja ya pesa. Nilitumia tu elf 72 na kuzika pesa mahali Fulani, nilipofika huko nilikuta pesa imeibiwa." Amesema Nafiu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags