Ajifungia kwa miaka 55 kisa kuogopa wanawake

Ajifungia kwa miaka 55 kisa kuogopa wanawake

Mwanaume mmoja kutoka nchini Rwanda aliyefahamika kwa jina la Callitxe Nzamwita mwenye umri wa miaka 71 amejitenga kwa miaka 55 akidai kuwa sababu ni kuogopa wanawake.

Inaelezwa kuwa Nzamwita alipokuwa na miaka 16 ndipo alipata tatizo hilo la kuwa na hofu pindi awaonapo wanawake na kuamua kuchukua uamuzi wa kujitenga mbali kidogo na kijiji ambapo alijenga uzio wa miti futi 15 uliozunguka nyumba yake huku ikielezwa kuwa toka aingie katika uzio huo hajawahi kutoka nje.

Hata hivyo, baadhi ya wanawake katika jamii hiyo wamejitahidi kumpelekea chakula na nguo kwa miaka yote hiyo lakini Nzamwita hakuwahi kufungua mlango bali huchukua vitu walivyovileta na kuviacha mlangoni na kuvitumia.

Kufuatia mahojiano yake alisikika akisema kuwa hataki wanawake karibu naye kwa sababu wanamtisha na anauzio unaozunguka nyumba yake kuhakikisha wanawake hawamkaribii.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BirudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags