Aingia na maiti benki ili apate mkopo

Aingia na maiti benki ili apate mkopo

Mwanamke mmoja kutoka nchini Brazil aitwaye, Érika de Souza Vieira ameshikiliwa na polisi baada ya kupeleka maiti ya mjomba wake Paulo Roberto Braga (68) benki ili kwenda kuchukua mkopo kwa jina la marehemu huyo kiasi cha dola 3,250 sawa na Sh 8 milioni.

Kufuatia na video pamoja na picha zinazosambaa mitandaoni zimemuonesha mwanamke huyo akimshikisha kalamu marehemu huyo huku akimsihi aweke saini kwenye karatasi ya benki.

Maofisa wa benki walishitushwa baada ya kuona mwili wa mteja huyo ukiwa umepauka sana ndipo wakaamua kuita jeshi la polisi ambapo mwili huo ulikaguliwa na kugundulika kuwa hauko sawa.

Mwanamama huyo ameshtakiwa kwa kosa la kukiuka sheria inayolinda maiti na kujaribu kuiba na kujipatia pesa kwa njia ya ulaghai, huku polisi nchini humo wakiendelea na uchunguzi kama kuna watu wengine wanahusika na tukio hilo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags