Aina za lipstick na utumiaji wake

Aina za lipstick na utumiaji wake

Bwana bwana leo katika kipengele chetu cha fashooon, enyi wadada sio mnapaka paka tuu lipstick lazima ujue aina zake shoga angu!.

Lipstick ni kipodozi chenye rangi ambacho mara nyingi hupakwa mdomoni na ipo katika muundo wa kimti (lip-mdomo, stick-mti). Lipstick zipo za aina na rangi na zina faida tofauti tofauti kwanza tutaanza na aina za lipstick,

(a). Lipstick za mafuta – hizi ni zile zenye mafuta hazichukui muda kufutika, lakini ni nzuri kwa ngozi ya midomo yako hasa kwa wale wenye midomo mikavu husaidia kuto kubabusha ngozi. Kwa sababu hizi ndizo zilikua za kwanza kabla ya kavu ndani yake kuna aina mbali mbali za lipstick lakini zote kwa ujumla uitwa lipstick za mafuta.

(b). Lipstick kavu – hizi hazina mafuta kabisa ukipaka zina kaa kwa muda mrefu sana na pia hufanya upate muonekano natural na bold. kwa sasa ndizo hutumika sana

Faida za Lipstick

  • uzuri- lipstick zinakupa muonekano mzuri usoni, ukiwa umepaka lipstick ya rangi yoyote ile ina kuongezea uzuri wako katika uso pia kama una hitaji kusimama mbele za watu au una hitaji kujiongezea kujiamini basi Lipstick ndio jibu lako.
  • Kuipa midomo/lips yako unyevu – kutokana na kuwa na mafuta na baadhi ya kemikali zenye mafuta na afya Lipstick zina saidia kuipa midomo yako unyevu ambao husaidia kuto kuharibika kwa midomo yako (mf; kubabuka midomo).
  • Jua – midomo ipo usoni kuikinga na jua ni kazi sana ni hadi uvae kofia lakini ni vipi endapo sehemu unazo tembelea mara kwa mara hazikuruhusu wewe kuvaa kofia? ni vyema ukapaka lipstick ili kuzuia midomo yako kuharibika na jua, baridi au hata upepo ambapo vitu hivi vinaweza kuiletea midomo yako madhara.

lipstick   zina kemikali mbali mbali ambazo zinaweza kusaidia kuikinga midomo yako na baadhi ya magonjwa.

Namna nyingine ya kutumia Lipstick

japo ime zoeleka lipstick hutumika katika midomo tu kuna namna nyingine ambapo lipstick ina weza kukusaidia

 

1) kuifanya kuwa highlighter

inaweza ikawa umesahau kubeba highlighter yako lakini kwenye pochi una lipstick yenye rangi ya highlighter labda rangi ya brown, unaweza kuitumia kama highlighter na ika kupa matokeo mazuri.

2)Lipstick  kama eyeshadow

pia una weza kutumia lipstick kama eyeshadow na ika pendeza tu aina yoyote ya lipstick ina pendeza kuwa kama eyeshadow iwe lipstick kavu au ya mafuta lakini ni vizuri pia ukatumia zile rangi za kuonekana zaidi kama nyekundu, blue nk.

3) Lipstick kama tattoo

inaweza ikawa una penda tattoo lakini hupendi kuchora, unaweza kutumia Lipstick kwa kujichora vizuri kama tattoo na baadae ukatoa

 Eeeeeh! wafuatiliaji wa mwananchi scoop msisahau kulike na kushare ili kupata dondoo za urembo na mitindo kama yooote

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post