Ahmedy: Mlitaka Mayele abaki kwenye timu yenu ili afe masikini

Ahmedy: Mlitaka Mayele abaki kwenye timu yenu ili afe masikini

Msemaji wa Klabu ya Simba Ahmed Ally ameingilia kati tabia ya baadhi ya mashabiki kumshambulia kwa maneno aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo Fiston Mayele.

Hayo yote ni baada ya mchezaji huyo ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Pyramid Fc, kuchoshwa na meneno ya baadhi ya mashabiki mitandaoni na kupelekea a-post picha kwenye mtandao wa Instagram na kuandika ujumbe akiuliza, chuki ya nini wakati yeye siyo Mtanzania au alikosea kucheza timu za Tanzania?.

Kutokana na post hiyo iliyoibua hisia za wadau wa mpira wa miguu akiwemo Haji Manara akimtaka Mayele afute alichoandika pia Ahmedy Ally ametoa neno.

Ahmedy Kupitia ukurasa wake wa Instagram amewataka mashabiki waache ushamba, huku akidai kuwa walitaka Mayele abaki kwenye timu hiyo ili afe masikini. Ahmedy ameandika,

"Mashabiki wa Nyuma Mwiko hebu acheni ushamba. Mlitaka Mayele abaki kwenye timu yenu ili afe masikini?. Yaani mpaka leo hamjazoea kuwa wachezaji wanakuja na kuondoka?

Pamoja na kuandika hayo Ahmedy amewatuhumu viogozi wa timu hiyo kuwa wao ndiyo wameanzisha chuku hizo,

"Sisi tunafahamu hii chuki haijaanzia kwa mashabiki imeanzia kwa viongozi wao, wakati unataka kuondoka walikufanyia mambo mengi ya hovyo ikiwemo kutuma watu wakuumize ili deal la kuhama lishindikane lakini Mungu alisimama na wewe.

Wewe siyo wa kwa kwanza kukufanyia hivyo ningetaja wengi lakini mfano wa karibuni ni Feisal Salum. Cha ajabu wanakuchukia wewe lakini wanatumia style yako ya kushangilia mpaka leo. Nyuma Mwiko mnatukanisha mpira wa Tanzania, meachwa kubalini acheni chuki

Aidha Ahmedy amewataka mashabiki kuacha fikra potofu huku akimpa pole Mayele kwa yanayomsibu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags