Ahmed: Kauli mbiu ya kwanza ya ‘klabu’ kutamkwa na rais wa FIFA

Ahmed: Kauli mbiu ya kwanza ya ‘klabu’ kutamkwa na rais wa FIFA

Msemaji wa ‘klabu’ ya #Simba #AhmedAlly ameanza tambo zake baada ya ku-posti video ya Rais wa #FIFA, Infantino kutamka kauli mbiu ya ‘klabu’ hiyo kwa kueleza kuwa rais huyo hakufundishwa bali anaijua kauli hiyo toka zamani.

Kupitia ukarasa wa Instagram wa #AhmedAlly ame-share video hiyo iliyoambataniashwa na na ujumbe ukieleza kuwa sio kama Infantino amefundishwa kauli hiyo bali anaijua toka zamani huku akidai kuwa ndio kauli mbiu ya kwanza ya ‘klabu’ kutamkwa na raisi wa #FIFA.

#Infantino alitamka kauli hiyo ya ‘Simba nguvu moja’ katika mchezo wa ufunguzi wa ‘Ligi’ ya Soka Afrika, (AFL) siku ya jana ambapo ‘klabu’ ya simba ilikipiga dhini ya #AlAhly kutoka nchini #Misri huku ‘mechi’ ikimalizika kwa goli 2-2.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags