Ahmed Ally: Tunahitaji mfungaji bora

Ahmed Ally: Tunahitaji mfungaji bora

Baada ya kiungo wa Simba, Saido Ntibazonkiza kumsogelea kwa ufungaji mshambuliaji Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 16 na yeye 15, uongozi wa Simba umetoa neno.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wanakitaka kiatu cha ufungaji bora msimu wa 2022/23 na mechi ya mwisho ya msimu watamsaidia Saido ili akibebe.

Ligi Kuu Bara imebaki mechi moja kutamatakika ambapo Simba itacheza dhidi ya Coastal Union Dar na Yanga itacheza dhidi ya Tanzania Prisons Sumbawanga.

“Tunahitaji mfungaji bora, zimesalia bao 2 na hakuna mashaka kwenye mechi ya mwisho ya Coastal tutamsaidia timu nzima awe mfungaji bora”

“Uliona kuna nafasi John Bocco alikuwa nafasi ya kufunga akasema hii ya Saido akamwekea akafunga, bao la tano alikuwa na uwezo wa kufunga Kibu lakini akamtengea Saido” amesema Ahmed Ally






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags