Ahmed Ally: Tukutane uwanja wa Uhuru tuagane

Ahmed Ally: Tukutane uwanja wa Uhuru tuagane

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi leo kwenye mechi ya kufungia msimu 2022/23 dhidi ya Coastal ili watumie fursa hiyo kuwaaga wachezaji na wachezaji wawashukuru mashabiki licha ya kukiri kwamba hakuna walichovuna kwakuwa Simba hana Kombe lolote msimu huu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Meneja huyo ameandika kuwa “Baada ya safari ndefu hatimaye leo tunafikia ukingoni, tulitamani safari yetu tuimalize kwa furaha lakini haijawa hivyo lakini hiyo haitupi sababu ya kuacha kuipa support Timu yetu pendwa”

“Wana Simba tukutane Uwanja wa Uhuru leo saa 9:30 tuwaage Wachezaji wetu na Wachezaji watuage sisi, japo hakuna tulichovuna tuwapongeze kwa kazi kubwa waliyoifanya na wao watushukuru kwa kuwashangilia katika nyakati zote “

“Pia sisi kama Familia ya Mashabiki tupate nafasi ya kuagana na kutakiana heri ya mapumziko, na tunawapenda sana” ameandika Ahmed Ally






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags