Ahmed Ally: Simba kama dhahabu ya moto

Ahmed Ally: Simba kama dhahabu ya moto

Siku moja baada ya kipigo cha pili mfululizo kutoka kwa ‘klabu’ ya #Yanga, Meneja habari na mawasiliano wa ‘klabu’ ya #Simba #AhmedAlly ameibuka kuwatia moyo mashabiki wa ‘timu’ hiyo.

Kupitia ukurasa wake wake wa #Instagram, Ahmed ame-post picha za wachezaji wa Simba ikiambatana na ujumbe wa kuwatia moyo mashabiki kwa kueleza kuwa hata dhahabu hupitishwa kwenye moto mkali ili ipate thamani na iwe bora.

Hivyo ameeleza kuwa mashabiki wa Simba wavumilie kupitia kwenye moto mkali huku akidai kuwa mapito hayo wanayoyapitia yanawafanya wawe bora na hadhi yao irudi tena kama ilivyo dhahabu.

Ikumbukwe kuwa ‘klabu’ hiyo ilifungwa mabao 2-1 dhidi ya ‘klabu’ ya Yanga siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags