Ahmed Ally: Mzungu sina mashaka nae atafunga sana huyu

Ahmed Ally: Mzungu sina mashaka nae atafunga sana huyu

Aloooooooh! Naona watani wanavyo tambiana bwana, baada ya klabu ya yanga kumrudisha tena mchezaji wao mwenye mbio za swala TK master Kisinda, mzee wa mlete mzungu hakukaa kimya bwana nayeye akaamua kuongea yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram semaji la simba aliandika “Mlete Mzungu katika mechi mbili za ligi kuu ya NBC amefunga goli 1. Ndio mshambuliaji pekee aliyefunga bao kwa kucheza dakika chache zaidi kwenye ligi, Dakika 27 tuu” aliendelea kwa kuandika kuwa

“Washambuliaji wengine katika vilabu vyao imewalazimu kucheza zaidi ya dakika 90 kufunga bao moja hivyo basi Sina mashaka nae atafunga sana huyuuuu” ameandika Ahmed Ally

Nyie nyie vita bado mbichi kwa watani hawa, waswahili wanasema wacha muda uongee, dondosha komenti yako hapo chini kwa kuzungumzia alicho kiandika msemaji je ni chakweli au laaah.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags