Ahmed Ally: Mpinzani aliye baki ni Yanga

Ahmed Ally: Mpinzani aliye baki ni Yanga

Msemaji wa ‘klabu’ ya #Simba, #AhmedAlly amedai kuwa mpinzani wao aliye baki ni watani wao #Yanga ambaye wanashauku ya kumfunga.

Akizungumza na waandishi wa habari Ahmed ameeleza kuwa ‘mechi’ hiyo dhidi ya watani wao ni ‘mechi’ ambayo wanaisubiri kwa hamu kuanzia kwa mashabiki ‘benchi’ la ufundi, wachezaji na viongozi.

 Huku akidai kuwa ‘timu’ yake ikishaifunga ‘klabu’ ya Yanga itakuwa imemaliza kila kitu ambapo anaeleza kuwa shughuli yao itakayo baki ni kukamilisha ratiba ya msimu.

‘Mechi’ hiyo ya watani wa jadi inatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili Novemba 5 mwaka huu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags