Ahmed Ally: Mashabiki kuweni watulivu

Ahmed Ally: Mashabiki kuweni watulivu

Baada ya ‘klabu’ ya #Simba kupokea kipigo kizito cha bao 5-1 dhidi ya ‘klabu’ ya #Yanga siku ya jana, Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ‘klabu’ ya Simba, Ahmed Ally amewataka mashabiki kuwa watulivu na kuwapa viongozi, ‘benchi’ la ufundi na wachezaji wao utulivu wa kujitathmini kwa maslahi ya ‘mechi’ zijazo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ahmed amesema kuwa ‘mechi’ ya jana ni moja kati ya ‘mechi’ ambayo huwa inaacha furaha ya kudumu au huzuni ya kudumu kwenye mioyo ya mashabiki.

Aliendelea kueeleza kuwa mashabiki wa ‘timu’ hiyo kuwa watulivu bila kuleta lawama yoyote kwa viongozi, benchi la ufundi na wachezaji, huku ikitaka wajiandae kwa ajili ya ‘mechi’ zijazo.
.
.
.
#MwanachiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags