Ahmed Ally, Manzoki sio mchezaji wetu

Ahmed Ally, Manzoki sio mchezaji wetu

 Haya haya wale mashabiki mliokuwa mnamsubiri sana yule mchezaji wa Vipers Sc Manzoki, sasa bwana yule mzee wa mletee mzungu ameamua kufunguka na kusema kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya timu aliokuwepo

Ahmed ameyasema hayo katika moja ya chombo cha habari akiwa katika mahojiano na kusema kuwa ““Tunamtamani Cesar Lobi Manzoki , ni mchezaji mzuri amefanya makubwa sana ligi ya Uganda akiwa na Vipers SC takwimu zake hazidanganyi ni mchezaji ana uwezo wa kukupa kila kitu unachokihitaji.”Amesema Ahmed Ally.

Aidha msemaji huyo aliendelea kwa kusema kuwa usajili baina ya mchezaji huyo na Simba SC haujakamilika hivyo mchezaji huyo bado ni mali ya Vipers SC, niwaambie tuu wanasimba hadi hii leo Manzoki sio mchezaji wetu.

Duuuuuuuuh! Mashabiki wa simba kindaki ndaki punguzeni presha kidogo ni swala la muda tuu, dondosha komenti yako hapo chini mtu wangu wa nguvu, na usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa Zaidi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags