Ahmed Ally: Hatuna cha kujivunia msimu huu

Ahmed Ally: Hatuna cha kujivunia msimu huu

Ikiwa ni usiku mmoja umepita baada ya tuzo kwa waliofanya vizuri msimu wa 2022/23 kutolewa, Meneja Habari wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema washahitimisha rasmi msimu.

Kupitia Instagram Ahmed amewapongeza waliotwaa ubingwa na waliopata tuzo na wasimamizi wa ligi pamoja na waaandaji wa tuzo.

"Kwetu Simba tuwapongeze nyota wetu waliotwaa tuzo hakika wametuheshimisha. Kiujumla kama timu hatuna cha kujivunia sana maana hatujapata tulichokihitaji msimu huu," ameandika Ahmed na kuongeza

"Hii inatupa nafasi ya kujipanga zaidi kwa msimu ujao. Ubingwa unahitaji wachezaji bora na timu imara. Ni jukumu letu viongozi kutafuta wachezaji sahihi na kutengeneza timu madhubuti, na hilo limeshaanza kufanyika kwa umaridadi wa hali ya juu sana," ameandika Ahmed

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags