Ahama kwa wazazi na kwenda kuishi kwenye treni

Ahama kwa wazazi na kwenda kuishi kwenye treni

Kijana mmoja kutoka nchini Ujerumani aitwaye Lasse Stolley (17) anadaiwa kuhama kwa wazazi wake na kwenda kuishi katika treni za ‘Deutsche Bahn’ kwa mwaka mmoja na nusu sasa.

Stolley alihama kwa wazazi wake akiwa na miaka 16 hapo awali ilikuwa ni ngumu kwa wazazi kukubali lakini baadaye wazazi wake walikubali kumuunga mkono kwenda kuishi maisha yake ya pekee.

Inasemekana kuwa Lasse hutumia dola 9,000 ambayo ni zaidi ya tsh 22 milioni kwa mwaka pesa ambayo anatumia kununua tiketi.

Kufuatiwa na mahojiano yake ya hivi karibuni ameeleza kuwa japo maisha ndani ya treni siyo ya faragha lakini ana-enjoy kuishi humo ambapo ameweka wazi kuwa usiku hulala kwenye treni inayotembea ya Intercity Express (ICE) na wakati wa mchana anakaa kwenye viti na kufanya kazi kama mtayarishaji program.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags