Agharamikiwa harusi na KFC baada ya kumchumbia mpenzi wake kwenye mgahawa wao

Agharamikiwa harusi na KFC baada ya kumchumbia mpenzi wake kwenye mgahawa wao

Mwandishi wa habari mmoja kutoka Nchini South Africa alishangazwa na kitendo cha jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Hector Mkansi kwa kumvisha mpenzi wake pete ya uchumba kwenye mgahawa wa KFC, lakini hali imekua tofauti baada ya kampuni hiyo ya chakula kureply tweet hiyo na kuomba wapewe mawasiliano ya mhusika ili wadhamini ndoa yao.



Baada ya KFC kujitokeza pia kampuni ya cocacola wametoa udhamini wa vinywaji kwenye sherehe yao huku kampuni ingine inayo jihusisha na utengenezaji wa pete ilisema itagharamikia pete za ndoa, na kampuni ya magari ya Audi walisema watadhamini safari za wakati wa honey moon.

Kupitia post ya mwandishi huyo alietaka kumcheka jamaa amejikuta amewasaidia kupata udhamini wa kila kitu kinachohusu ndoa yao. Ndo maana siku zote waswahili wanasema usiogope kuchekwa maana ndipo mafanikio yanapo tokea.

Hahahahah! Kula chuma hicho, wakati mwingine mungu hutupa kwa njia ya tofauti nan do maana kesho yetu ni fumbo so tusizarauliane.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags