Afumwa akijaribu kuchoma nyumba aliyozaliwa Martin Luther King

Afumwa akijaribu kuchoma nyumba aliyozaliwa Martin Luther King

mwanamke mwenye umri wa miaka 26 anashikiliwa na polisi kwa kutaka kuchoma nyumba aliyozaliwa na kukulia Martin Luther King Jr. kwenye barabara ya Auburn, Atlanta.

Inaelezwa kuwa mwanamke huyo jana usiku alionekana akimwaga petroli na kujaribu kuchoma nyumba hiyo ya mmoja kati ya wakombozi wa watu weusi, katika tukio hilo Maafisa wawili wa Idara ya Polisi ya Atlanta waliweza kumuweka chini ya ulinzi.

Aidha Mkuu wa Polisi wa Atlanta Darin Schierbaum amesema kuwa endapo mwanamke huyo angefanikiwa kutekeleza tukio hilo basi angekuwa amepoteza sehemu muhimu ya historia ya Marekani.

Martin Luther King Jr alikuwa Waziri wa Kibaptisti wa Marekani, mwanaharakati, na mwanafalsafa wa kisiasa ambaye alikuwa mmoja wa viongozi mashuhuri katika harakati za kupigania haki za watu weusi tangu 1955 hadi kuuawa kwake mwaka 1968.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags