Seneta wa Kenya Gloria Orwoba alifukuzwa bungeni baada ya kuhudhuria kikao akiwa amevalia suti nyeupe iliyokuwa na alama za rangi nyekundu (kuashiria hedhi) katika kampeni inayoonekana kuwa ya harakati za kushinikiza upatikanani wa taulo za hedhi.
Mbunge huyo anatarajiwa kuwasilisha hoja kuhusu mswada wa kutoa taulo za kike bure siku ya Jumatano kama sehemu ya juhudi za kumaliza umaskini wa muda.
Spika wa bunge Amason Kingi aliamuru seneta huyo kwenda kubadilisha nguo zake kabla ya kuruhusiwa tena bungeni.
“Sio kosa kuwa na hedhi Seneta Gloria nasikitika unapitia hali ya kimaumbile, suti yako imepata madoa ya ajabu, naomba uondoke ili ukabadilishe urudi na nguo ambazo hazina madoa” amesema Spika
Seneta Orwoba aliwaambia waandishi wa habari “Tunalenga kutokomeza janga linalotokana na unyanyapaa wa hedhi. Baadhi ya mambo ambayo ninayotetea na kubuni sheria na kuhakikisha kwamba tunatoa bure taulo za hedhi kwa watoto wote wanaokwenda shule” amesema Gloria Orwoba
Leave a Reply