Afariki kwa kula uyoga ulioota nyuma ya nyumba yake

Afariki kwa kula uyoga ulioota nyuma ya nyumba yake

Mwanamume mmoja aliyefahamika kwa jina la William Hickman mwenye umri wa miaka 55 anadaiwa kufariki baada ya kula uyoga wenye sumu uliokuwa umeota nyuma ya nyumba yake katika kijiji cha Windham kilichopo kwenye jimbo la Ohio.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vimeeleza kuwa William alitumia program iitwayo ‘Plant Identifier’ iliyoko kwenye simu yake ya kutambua mimea yenye sumu ndipo programu hiyo ilitambua kimakosa kuwa uyoga huo unaweza kuliwa.

William alikimbizwa hospitali na familia yake na kufariki wakati alipokuwa akipatiwa matibabu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags